Balozi
wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer kizungumza
jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika
yasiyo ya kiserikali iliyofanyika jana. Picha na Geofrey Adroph
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais
akizungumzia masuala ya kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali ili ziweze
kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa maana hizo zinawalenga watu katika
jamii husika.
Mwakilishi
wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga akizungumza juu ya ushirikiano
wa Umoja wa Ulaya(EU) ulivyoamua kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali
za Tanzania Bara pamoja na Zanzibar. Maeneo ambayo Umoja wa Ulaya
inajikita nayo katika asasi zisizo za kiserikari ni tatu amabazo ni
kuweka mazingira bora kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi
katika mazingira bora hapa nchini, pili ni kuyajengea uwezo mashirika
hayo na mwisho nikufanya kazi katika Sere pamoja na sheria ili kuwa na
sheria bora na nzuri kwa maendelea ya nchi yetu.
Baadhi
ya mabalozi kutoka Umoja wa Ulaya(EU) pamoja na wageni waalikwa wakiwa
kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo
ya kiserikali iliyofanyika jana
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais(kulia)
akisaini kuashiria uzinduzi rasmi wa programu ya kusaidia mashirika
yasiyo ya kiserikali kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini
Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer(kushoto)
pamoja na Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga wakisaini
kuashiria uzinduzi rasmi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya
kiserikali za Tanzania Bara na Zanzibar. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja
wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais(kushoto),
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De
Geer(katikati) pamoja na Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis
Kiwanga wakizindua rasmi programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya
kiserikali za Tanzania Bara na Zanzibar.
Picha ya Pamoja.
0 comments: