Halmashauri
ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati 500 kutoka Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea
madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada
huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha
Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James
Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo
ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa
wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na
uendelezaji wa gesi na mafuta.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi.
Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia
wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri
ya Wilaya ya Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akionesha moja ya jezi ambayo
TPDC ilitoa msaada kwa timu ya Wazawa FC iliyopo kijiji cha Mngoji, na
Tagesh Academy zote za Mtwara.
Wachezaji wa timu
ya Wazawa FC wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt.
James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, Mbunge wa Mtwara
Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally na viongozi wengine baada ya kukabidhi msaada
wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tshs. 5,000,000/=
0 comments: