Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi.
Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za
Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba
(hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi.
Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya
Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na
taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar es Salaam.
KAMATI ya
Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kutekeleza
kwa vitendo ahadi zake za kuiwezesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
kujiendesha kibiashara. Akitoa maazimio ya Kamati ya PIC leo Dar es
Salaam baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini
TTCL, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge
wa Busanda) alisema, ili TTCL iweze kutekeleza jukumu lake kwa Taifa,
Serikali iharakishe utekelezaji wa ahadi zake kwa Kampuni hiyo Kongwe ya
Mawasiliano nchini. "Serikali ikamilishe kwa haraka mchakato wa
kuondoka kwa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL, mchakato huu
umechukua muda mrefu sana, ni vyema sasa ukatekelezwa sambamba na
kuisaidia TTCL kupata malipo yake inayodai kutoka kwa Wateja wake
zikiwemo taasisi za Serikali," alisema Bi. Bukwimba.
Aidha
Mhe Bukwimba aliongeza kuwa, Kamati ya PIC inaiagiza Serikali kupitia
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha mchakato wa
kukabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa TTCL ili utumike kibiashara
na kwa ufanisi zaidi kuliko hivi sasa ambapo umiliki wake haupo bayana. Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi.
Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za
Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.[/caption]
Alisema kwa kipindi cha miaka 15 hivi sasa Serikali haijafanya uwekezaji
wa aina yoyote ndani ya TTCL hivyo kuitaka kuwekeza ili kampuni iweze
kusonga mbele kibiashara. "...Kwasababu huwezi kutegemea kupata mapato
mazuri bila kuwekeza uwekezaji wa aina yoyote...miaka kumi na tano ni
mingi mi nauhakika wakiwekeza fedha wataweza kuisaidia kampuni kuiuwisha
na kuweza kufanya shughuli zake vizuri kama taasisi zingine.
."
Agizo jingine la PIC kwa Serikali ni kuiongezea TTCL wigo wa kutumia
rasilimali zake kama dhamana ili kupata mitaji kutoka taasisi za fedha
na kufanikisha mpango wa kampuni hiyo wa kufanya mageuzi ya kibiashara.
Awali, Wabunge waliochangia hoja katika kikao hicho, waliitaka Bodi na
Menejimenti ya TTCL kusimamia kikamilifu mipango mizuri ya kibiashara
iliyowasilishwa mbele ya Kamati. Wabunge Esther Matiko (Tarime Mjini),
Steven Ngonyani (Korogwe) Riziki Lulida (Viti Maalum), Sabrina Sungura
(Viti Maalum), na Frank Mwakajoka (Tunduma) wamesema, Seriki inao wajibu
mkubwa wa kuisaidia TTCL ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikipitia
kipindi kigumu hasa kutokana na uwekezaji usio na tija uliofanywa ndani
ya Kampuni hiyo.
0 comments: