Showing posts with label Favourite. Show all posts

Wednesday, May 4, 2016

http://nicemediaworkstz.blogspot.com/Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali sura 182 ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kwa wasafirishaji na watumiaji wa kemikali hapa nchini. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi na kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.
http://nicemediaworkstz.blogspot.com/Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za usafirishaji wa kemikali na madereva 123 hapa nchini. Kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.

Frank Mvungi-Maelezo

Serikali itatoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123 wanaosafirisha Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na matumizi yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura 182.

Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 matukio ya kemikali yalisababisha vifo 14.

“Jumla ya matukio 11 ya ajali za Kemikali yalitolewa taarifa katika kipindi cha mwaka jana pekee na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua moto magari na tani 250 za kemikali”.alisisitiza Mallya.

Akifafanua kuhusu matukio hayo Mallya amesema kuwa ajali hizo zilisababishwa na kukosekana kwa uelewa juu ya athari zinazoweza kusababishwa na kemikali hizo miongoni mwa wasafirishaji na watumiaji.

Kama sehemu ya utekelezaji wa sheria hii,Serikali inatarajia kuendelea kufanya mafunzo ya wadau kuhusiana na kemikali zenye kusababisha mlipuko.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa wakuu wa polisi wa Usalama barabarani nchi nzima yanalenga kuongeza uelewa kwa wadau wanaohusika katik a kutumia na kusafirisha kemikali ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.

Katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yasiliyo salama,ajali na matukio ya kemikali,Serikali iliamua kutunga sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura 182 (The Industrial and Consumer Chemicals Management and Control) Act Capt 182).

Lengo kuu la sheria hii ni kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyo salama bila kuleta athari kwa watu na mazingira.

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI

at 10:34:00 AM  |  No comments

Read More

Sunday, May 1, 2016

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
http://nicemediaworkstz.blogspot.com/Bw. John Cheyo mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
http://nicemediaworkstz.blogspot.com/Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.

http://nicemediaworkstz.blogspot.com/Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam

Na Monica Laurent -Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini ambalo linaundwa na wawakilishi wawili kutoka kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa .

Mapendekezo hayo yalitolewa na Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa udhamini wa UNDP kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini. Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini vikiwemo vyama vya siasa.

Akiwasilisha mapendekezo, Msajili Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa ilipendekezwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu wa kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro ndani ya chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa na kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa sehemu ya mapendekezo

“Upatanishi ukishindikana mgogoro husika uwasilishwe kwenye Baraza la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa Baraza la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa Baraza. Muhusika asiporidhika na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata rufaa Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.

Aidha kumekuwa na msisitizo wa kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama kwenda moja kwa moja Mahakamani ambako huchukua muda mrefu na kuathiri ukuaji wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.

Wakichangia katika mjadala huo, baadhi ya wajumbe walikubaliana na hoja kuwa vyama vya siasa vitatue kwanza migogoro yake ndani ya vyama na kwamba pale tu itakaposhindikana ndipo ipelekwe kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Wajumbe walishindwa kukubaliana katika hoja ya uwepo wa Baraza la Uamuzi wa Migogoro ya vyama vya siasa, wapo walioona haja ya uwepo wake na wapo walipendekeza kuwa majukumu ya Baraza hilo yafanywe na Baraza la Vyama vya siasa lililopo sasa jambo lililosababisha kutokukubaliana katika hoja hiyo.

Pamoja na michango iliyotolewa , Wajumbe wameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwekeza katika Baraza la Vyama vya Siasa ili kusaidia utatuzi wa migogoro nchini kwa kuwa imebainika kuwa machafuko katika nchi nyingi duniani yamesababishwa na machafuko katika masuala ya siasa.

Akihitaji ufafanuzi wa hatua gani imefikiwa katika uboreshaji wa Sheria ya Vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, Mhe. Peter Kugar Mziray aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ufafanuzi. Naye Msajili Msaidizi, Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi alisema tayari vyama vyote vya siasa vimeshapelekewa barua vikiombwa kuwasilisha mapendekezo kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na kwamba Ofisi inafanya jitihada za kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau wa siasa na ikishakamilisha upokeaji huo, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.

VYAMA VYA SIASA VIMEKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA MFUMO WA UTATUZI WA MIGOGORO NDANI NA BAINA YA VYAMA

at 12:51:00 PM  |  No comments

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.