Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw.
Elias Mwanjaa (kushoto) alipowasili katika uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine kuangalia mchezo kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga
jana Jijini Mbeya. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi
Makalla.Wachezaji
wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi
kabla ya kuanza mechi yao na Mbeya City jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya
City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.Wachezaji
wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union na Mbeya City wakisakata
kabumbu jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao
manne kwa sifuri.Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akifuatilia kwa makini mchezo wa mpira wa miguu kati ya Mbeya City na
Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya baada ya kumaliza ziara yake ya
kikazi jijini hapo. Kushoto kwa Mhe. Nnauye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Bw. Amosi Makalla na wakwanza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya
Ndg. Halhaji Kundya.Wananchi
wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia ushindi wa timu yao ya Mbeya City baada
ya kuichapa timu ya Coastal Union ya Tanga mabao manne kwa sifuri jana
katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya
0 comments: