Mhashamu
Askofu Izaac Amani wa jimbo katoliki la Moshi kwa masikitiko na huzuni
kubwa, anatangaza kifo cha mheshimiwa sana padre FABIAN NDERUMAKI, padre
wa jimbo katoliki la Moshi.
Padre Fabian Nderumaki alifariki dunia jana saa nne usiku.
Padre Nderumaki hadi mauti yanamfika alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Himo jimboni Moshi.
Kabla
ya kuteuliwa na baba askofu kuwa paroko wa Himo, padre Fabian Nderumaki
alikuwa Gombera (Rector) wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yakobo-Kilema
(St. James Seminary)
Tunatoa
pole kwa familia, ndugu jamaa, marafiki, wote waliofanya naye kazi
seminari ya St. James na waumini wote ambao Padre Fabian Nderumaki
amewahi kuwahudumia katika parokia zao kama padre enzi za uhai wake. Pia
kwa mapadre, watawa na wote waliowahi kufanya nae kazi
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe milele na milele, AMINA.
ROHO YA MAREHEMU PADRE FABIAN NDERUMAKI IPATE REHEMA KWA MUNGU, APUMZIKE KWA AMANI.
0 comments: