Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema MCC kuinyima fedha Tanzania ni
kwa sababu ya ubabe wa CCM na kwamba, sasa watu wasivikwe koti la
uzalendo kwa jambo hilo.
Kwenye
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Zitto aliandika kuwa:
“Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi
waliochagua viongozi wao Oktoba 25, 2015.
“Sitakubali
kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM,
kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar.
“Haina
mahusiano yeyote na uhuru wa nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na
subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. Nawasihi Watanzania
kuelewa kwamba CCM ndio imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila
kuufanya ni mzigo wa nchi.”
Aliandika
pia kwamba: “Zanzibar inatazamwa kama Zanzibar, kwa wenye maono mafupi.
Nilipata kuwaambia viongozi wenzangu kwamba tishio kubwa zaidi la
kutoshughulikia mtanziko wa Zanzibar ni upotoshaji.
“Tutajikuta
tunaacha kushughulika na masuala ya maendeleo kwa kipindi kirefu
kidogo. Tabia ya kitanzania ya kupenda ‘shortcuts’ (njia za mkato)
itatugharimu sana. You can’t just ignore Zanzibar and move on. You just
can’t (huwezi ukaipuuzia Zanzibar na ukaendelea tu, huwezi).”
Pia Mbunge huyo aliandika kuwa: “Serikali ya Marekani imesitisha mahusiano na Serikali ya Tanzania kwenye miradi ya MCC.
“Hivyo Tanzania itakosa Sh. trilioni moja ambazo zilikuwa zimeelekezwa kwenye umeme na umeme vijijini.
“Sababu?
Zanzibar na Cybercrime Act. Siku si nyingi tutawasikia Umoja wa Ulaya
nao. Nasubiri kusikia Serikali ya Rais Magufuli itasema nini.
“Suala
la Zanzibar likitazamwa kibabe kwa kuwa watawala wana maguvu nchi
itaingia kwenye matatizo makubwa sana ya ndani bila kujali misaada
inakatwa au la. Sipendi misaada. Sipendi mataifa ya kigeni kuingilia
masuala yetu ya ndani.
“Lakini
Tanzania sio kisiwa, tunaishi ndani ya jamii ya kimataifa. Kuna mambo
lazima tufanye kwa kuzingatia misingi ya kidunia. Zanzibar ni moja ya
jambo hilo. Tusiweke kichwa kwenye mchanga kama mbuni.”
Naye
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje wa Chama
Cha ACT-Wazalendp, Theopister Kumwenda, alisema uamuzi huo wa MCC
utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua
na umaskini.
Alisema
ACT-Wazlendo inatambua kuwa katika kipindi hiki Tanzania inahitaji
mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo
duniani, likiwamo MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo.
Alisema MCC imekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijijini
0 comments: