Mkulima
wa vitalu vya karafuu wa Kitope Mzee Sheha Khamis akimuelezea
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ZSTC changamoto anazokabiliana nazo
katika kutekeleza kazi hiyo wakati Mkurugenzi huyo alipofanya ziara
katika Mkoa Kaskazini Unguja na Wilaya Kati.
Mfanyakazi
wa kitalu cha Mikarafuu cha Donge Bi Fatma akitayarisha udongo kwa
ajili ya kuatika miche katika shamba hilo linalomilikiwa na Wizara ya
Kilimo na Mali Asili.
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Shirika
la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kwa kushirikiana na Wizara ya
Kilimo na Mali Asili linakusudia kuongeza mashirikiano na kuwasaidia
wananchi wanaoanzisha vitalu vya mikarafuu Unguja na Pemba.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa ZSTC Bibi Mwanahija Almasi ametoa ahadi hiyo baada ya
ziara yake ya siku mbili kutembelea vitalu vya mikarafuu vya Serikali na
vya watu binafsi katika vijiji vya Kitope, Kidimni, Machui Selem na
Donge kuona matatizo yanayowakabili katika kutekeleza kazi zao.
Amesema
vitalu vya watu binafsi vinamchango mkubwa katika kuimarisha zao la
karafu Zanzibar kwa kuziba pengo linalojitokeza wakati wa ugawaji wa
miche ya mikarafuu kwa wakulima kutoka vitalu vya Serikali
Amesisitiza
kuwa kutoakana umuhimu huo na kazi kubwa wanayochukua wakulima hao
huku wakikabiliwa na upungufu wa nyenzo muhimu, Shirika litatoa
pembejeo zitakazosaidia kufanikisha kazi zao kwa ufanisi.
Wakati
wa ziara hiyo wakulima wanaomiliki vitalu vya mikarafuu walimueleza
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC kwamba wanakabiliwa na tatizo la vifuko
vya kuatikia miche (policing), mabero, pauro na maji hasa wakati wa
kiangazi.
0 comments: