Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa
Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali
kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika
iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es
Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za
kitanzania.
.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana
Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka
jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
Balozi wa Korea nchini Geum-young Song (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.
MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na balozi wa Korea nchini Geum-young
Song wameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika Manispaa ya Ilala
jijini Dar es Salaam ambapo itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa
kuhudumia wananchi 4000.
Akizungumza
katika hafla ya kuweka jiwe hilo la msingi Chanika jijini Dar es Salaam
jana, Makonda aliishukuru serikali ya Korea kwa msaada wa ujenzi wa
Hospitali hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa Chanika na kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Amana.
"Tunawashukuru
hawa ndugu zetu wa Korea Kusini kwa msaada wa kutujengea Hospitali hii
nawaombeni wananchi kuitunza ili kila mtakapokuwa mnafika kutibiwa
tuwakumbuke wakorea" alisema Makonda.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victorina Ludovic alisema ujenzi wa
Hospitali hiyo utasaidia kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi
wapatao 398,882 kutoka maeneo ya Chanika, Msongola, Zingiziwa na Majohe
hivyo kupunguza muda na gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitumia
kufuata huduma hizo umbali wa kilometa 30 kwenda hospitali ya Amana ya
Rufaa.
Ludovic
alisema ujenzi wa mradi huo hadi utakapokamilika utagharimu dola la
milioni 4 sawa na sh.bilioni 8.8 za kitanzania.Balozi wa Korea nchini ,
Geum-young Song amesema wakorea hawafurahishwi wanapoona mama na mtoto
wanapoteza maisha wakati wa kujifungua nchini Tanzania.
"Nchi
yetu kupitia shirika la Koica imeamua kujitolea kujenga hospitali hii
ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora ya afya ya mama
na mtoto wakati wa kujifungua kwani hatupendi kuona wanapoteza maisha
wakati wa kujifungua" alisema Young Song.
Wananchi wa Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali yao.
Diwani
wa Kata ya Chanika, Mr Massaburi akitoa neno la Shukurani kwa RC
Makonda, Serikali pamoja na Serikali ya Korea kwa ujenzi wa Hospitali
hiyo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wasanii wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wa Manispaa ya Ilala na Korea Kusini.Na Dotto Mwaibale
0 comments: