Thursday, March 17, 2016

LAFARGE TANZANIA YATOA SARUJI MIFUKO ZAIDI YA 1,000 KUJENGA UPYA MABWENI SEKONDARI YA IYUNGA.

at 11:01:00 AM  |  No comments

Viongozi wa kampuni ya saruji ya Lafarge wakiwa pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya mabweni yaliyoteketea ya shule ya Sekondari Iyunga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro(kushoto) akipokea mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Meneja Uajiri watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge Bryson Tarimo kwa ajili ujenzi wa mabweni ya shule ya Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni.
Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya jijini Mbeya Bryson Tarimo akizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa moto,Kampuni ya Lafarge imetoa mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 14.

Mkuu wa shule ya sekondari ya Iyunga Edward Mwantimo akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa mifuko 1,000 ya saruji kutoka kampuni ya Lafarge ya jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa moto ambapo pia alielezea madhara yaliyotokana na moto uliosababisha kuungua kwa mabweni ya wanafunzi wa shule hiyo.

Share
, Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.