Kaimu Kamishina wa Fedha na Utawala, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IDARA ya Uhamiaji imefanya mabadiliko ya wafanyakazi katika vituo vya kazi ikiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi wa idara hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishina wa
Fedha na Utawala, Abbas Irovya amesema mabadiliko hayo ni kuongeza
ufanisi kazi na tija.
Mabadiliko
hayo ni DCI.Faustine Nyaki Mkoa wa Iringa anahamia Mkoa Mwanza, na
aliyekuwa Mwanza,DCI.Remigius Ibrahim Pesambilia anahamia kwenda kwa
Mfwadhi wa Ofisi ya uhamiaji uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere , DCI.Rose Mhagama (Njombe) amehamia Mtwara,DCI.Chale,s Habe
(Geita) anahamia Njombe.
Amesema kuwa mabadiliko hayo kwa wafanyakazi katika idara hiyo ni 200 ambapo inatokana agizo la Waziri mwenye dhamana hiyo.
0 comments: