Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye akizungumza na waandishi wa habari juu ya
mpango kazi wa Taifa wa dawa,vifaa tiba, na vitendanishi hasa katika
ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kudhibiti wizi wa dawa pamoja na
uwajibikaji,mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mfamasia
wa Serikali, Bw. Henry Irunde akifafanua jambo kwa waAndishi wa habari
jinsi ya kuwezesha udhibiti wa wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji, leo
jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
Wizara
ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imezindua mpango
mkakati wa Taifa wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi hasa katika ngazi
ya Halmashauri kwa lengo la kuboresha huduma ya afya katika Halmashauri
hizo.
Akizungumza
katika mkutano wa uzinduzi leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki
Ulisubisye amesema kila dawa katika Halmashauri husika itakuwa na nembo
pamoja na takwimu za watumiaji kwa lengo la kukwepa wizi wa dawa na
kuwapa taarifa wawekezaji kwa kuweka viwanda vya dawa za binadamu.
Katibu
Mkuu huyo,Bw.Ulisubisye ameongeza kuwa ukaguzi wa dawa utakuwa
endelevu,usimamizi wa vifaa pamoja na kuona utoaji wa huduma za afya kwa
mpango huo una ubora mkubwa.
Hata
hivyo, Wizara ya Afya imeeleza kuwa mpango huo utadumu kwa miaka mitano
hasa katika kutekeleza mpango wa dawa kupatikana katika kila
Halmashauri pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watoaji huduma za afya.
0 comments: