Baada ya kufichuliwa kutoka alipofichwa, mtoto huyo alionekana kuwa dhaifu kiafya kutokana na kukosa lishe pamoja na mazingira aliyokuwa akiishi kutoridhisha, jambo ambalo ni kosa kisheria, pia ukiukwaji wa haki za watoto.
Na Hamida Shariff, Morogoro.
Wakati jamii ikiwa bado haijasahau
mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na kusababisha kifo chake, tukio
lingine la aina hiyo limetokea katika Kijiji cha Matongola, Tarafa ya
Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya kubainika mtoto wa miaka sita akiwa
amefichwa uvunguni mwa kitanda na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama
yake mzazi.
Alisema kuwa mpaka sasa bado haijafahamika kama mtoto Davota ni mlemavu au la na kwamba taarifa za afya ya mtoto huyo zitatolewa baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi wa kina
0 comments: