Na Editha Karlo wa blog ya Jamii, Kigoma
MBUNGE
wa Jimbo la kigoma Kusini ,Hasna Mwilima amewakabidhi msaada wa
shilingi milioni sita na laki tatu na tani kumi na saba za vyakula kwa
wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Kirando kata ya Sunuka Wilayani
Uvinza.
Akizungumza
na Wananchi wa kijiji hicho wakati akikabidhi misaada hiyo iliyo tolewa
na Halmashauri ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma na wadau mbalimbali alisema
serikali kwa kuwathamini wananchi imeamua kutoa misaada ilikuweza
kuwasaidia wahanga waliopoteza mali zao wakati wa mafuliko.
Mwilima
alisema anaupongeza uongozi wa Mkoa wa kigoma na halmashauri zote kwa
kutoa msaada wa vyakula vitakazo wasaidia waathirika hao katika kipindi
hika ambacho wanajipanga kurekebisha makazi yao.
Pia
aliishukuru Halmashauri ya Uvinza kwa kuthamini Wananchi wake na kutoa
msaada wa shilingi milioni tano na Mwenyekiti wa Halmashauli hiyo
kuongezea laki mbili wameonesha jinsigani serikali ya awamu ya tano
inavyo wathamini wananchi.
“mimi
kama mbunge wenu nitatoa shilingi milioni moja nitaongezea katika
mchango wa Viongozi wengine waliotoa tutahakikisha tunashirikiana katika
wakati waraha, wakati washida na nyakati zote tupo pamoja nitawahudumia
ipasavyo ndugu zangu “, alisema Hasna.
Hata
hivyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuchangia Chakula tani saba
kupitia michango iliyotolewa na Halmashauri zote za Mkoa ilikuweza
kuwasaidia Wanakijiji waliokumbwa na mafuriko.
Rehema
Hassani ni mmoja kati ya Wahanga wa mafuriko pia ni Mkazi wa Kirando
alisema kwaniaba yawanakijiji wenzake wanaishukuru Serikali pamoja na
Mbunge kwa kutoa misaada hiyo tunaimani itatusaidia na tutaweza
kujipanga upya na kuziendesha familia zetu.
Aliiomba
Serikali kuwapatia maeneo mengine waweze kujenga na kuondoka kuishi
mabondeni ambapo mvua kubwa ikinyesha maji hujaa mtoni na kuingia ndani
kupelekea mafuriko hivyo serikali igawe maeneo mengine yakuweka makazi.
Msaada
uliotolewa ni maharage kilo218,mchere kilo1240, unga , mihogo,mahindi,
mashuka kwaajili ya zahanati 218,na mafuta ya kupikia na chumvi na
shilingi milioni sita na laki tatu watakazo gawiwa wahanga wa mafuriko
hayo zilizo tolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali.
Mafuriko
hayo yalitokea tarehe 13 mwezi wa pili mwaka huu kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha uharibifu mkubwa wa mali na kaya zipatazo 49 kukosa mahali
pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.
Mbunge
wa jimbo la Kigoma kusini Husna Mwilima akimkabidhi fedha shilingi.
Milioni sita na laki tatu mwenyekiti wa kijiji cha Kirando Athumani
Chuma kwaajili ya wahanga wa mafuriko katika kijiji hicho.
Mhe. Hasna Mwilima akimkabidhi Bi rehema Issa mfuko wa sembe mmoja wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha kirando.
Mhe. Hasna akiteta jambo na muathirika wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
Sehemu
ya chakula tani kumi na saba zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la
kigoma kusini Hasna Mwilima kwa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha
Kirando.
Baadhi ya makazi ya wanakijiji cha Kirando yaliyokumbwa na mafuriko
0 comments: