Wednesday, April 2, 2014

MASANJA MKANDAMIZAJI MSANII MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA..SOMA HAPA.

at 1:23:00 PM  |  No comments


Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.

 
“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu. Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake. “Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.

 






http://themonthlyjob.com/?refcode=7918
  Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake. MAGARI SITA Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa. NYUMBA TATU BONGO Pia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.
 http://themonthlyjob.com/?refcode=7918
 Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana. - MASHAMBA KIBAO Msanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga. NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI? Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu. Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’. 

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.