Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na
wauzaji wa filamu za nje kuhusu kufuata sheria ya uuzaji wa filamu hizo
hapa nchini katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao
kati ya Serikali na wauzaji wa Filamu za nje(Hawapo Pichani)
kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Bodi hiyo Bw Tairo.
Mwenyekiti
wa wauzaji wa filamu za nje Bw Joseph Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa
kikao baina ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo kilichofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wauzaji wa Filamu za nje walioshiriki katika kikao kati yao na
Serikali cha kubadilisha sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini
kilichofanyika leo jijjini Dar es Salaam.
Na: Shamimu Nyaki
Kufuatia
kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini bila kufuata
Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya
biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia
kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Nnauye wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa Filamu hizo leo jijini
Dar es Salaam.
Amewataka
wauzaji hao kuwa na mkataba pamoja wamiiki wa kazi hizo ili waweze
kufanya biashara hiyo kwa uhalali kwakua Serikali itawasaidia kusimamia
utekelezaji wa mikataba hiyo na kurahisisha utekelezaji wa sheria
iliyopo.
“Lazima
mfuate na kutekeleza Sheria iliyopo kwakua mimi nipo hapa kuisimamia na
kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa”.Alisema Mhe.Waziri Nape.
Aidha
katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo ameongeza kuwa ni
lazima wauzaji wa filamu hizo kuhakikisha kuwa filamu wanazouza
zimehakikiwa na bodi ya filamu pamoja na COSOTA ili kudhihirisha ubora
wa kazi hizo na viwango vya hapa nchini.
“Ni
lazima muhakikishe kazi mnazouza zimeruhusiwa na Bodi ya filamu pamoja
na COSOTA na zinafuata madili ya hapa nchini’’.Aliongeza Bi. Joyce.
Ameongeza
kuwa bodi ya Filamu pamoja na COSOTA wapo tayari kuwasaidia kupata
haki miliki ya filamu hizo wanazouza kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya
kuruhusu filamu gani inastahili kuuzwa na ipi haistahili kuwepo sokoni.
Uuzaji
wa filamu za nje hapa nchini umechangia kwa kiasi kikubwa filamu za
hapa nchini kukosa soko hali inayochangia kudidimia kwa sanaa hiyo hapa
nchini ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana.
0 comments: