Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa matokeo ya ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla akiangalia baadhi ya vifaa tiba na dawa zilizo kamatwa katika operesheni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangallaameagiza
Baraza la Wafamasia pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA),kuwafikisha mahakamani wale wote waliokutwa na dawa za serikali
katika maduka yao.
Kigwangalla
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kupewa matokeo ya
Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na yasiokuwa na vibali
iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA pamoja na Jeshi la Polisi,
amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka katika hospitali za
serikali.
Amesema
kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika
maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.
Kigwangalla
amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa
ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo
inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.
Aidha
amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa
nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na
wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.
Operesheni
hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685
katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu
mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za
asili.
Aidha
Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa
malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo
wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi.
Kigwangalla
amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na
kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali
katika duka la dawa.
Amesema
kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote waliokutwa
na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa
dawa hizo.
0 comments: