Wakenya wenye asili ya Kisomali wamedai kuhangaishwa na maafisa
wa polisi kwenye oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka magaidi
waliohusika na shambulizi la guruneti katika mtaa wa Eastleigh mjini
Nairobi siku chache zilizopita.
Raia hao wamedai kwamba licha ya kuwa na vitambulisho vya taifa vinavyothibitisha kwamba wao ni Wakenya, polisi wameendelea kuwahangaisha na kuwatesa kwa madai kwamba wao ni al-Shabab.
Makundi ya kiraia yameitaka polisi ya Kenya kufuata sheria katika oparesheni hiyo na kutowahangaisha raia wasio na hatia.
Polisi ya Kenya imesema wengi wa raia wenye asili ya Kisomali wana vyeti bandia vya utambulisho na kwamba idadi kubwa ni wakimbizi wa Somalia waliotoroka kwenye kambi za Daadab na Kakuma.
Kwenye shambulizi la guruneti dhidi ya raia katika mtaa wa Eastleigh siku mbili zilizopita, watu 6 walipoteza maisha na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Hadi sasa hakuna mtu au kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo ingawa vyombo vya usalama Kenya vinalilaumu kundi la kigaidi la al-Shabab la nchini Somalia.

0 comments: