Serikali ya Mali imetangaza kuwa, yumkini virusi vinavyosababisha
ugonjwa wa Ebola vimeingia nchini humo kwani tayari watu 3 wameonyesha
dalili za ugonjwa huo.
Waziri wa Afya wa Mali, Ousmane Kone, amesema uchunguzi zaidi unafanywa ili kubaini iwapo virusi hivyo vimeingia katika nchi hiyo. Nchini Liberia nako, serikali imetangaza kuwa, mtu mmoja aliyefika hospitali kutafuta matibabu anaonyesha dalili za kuambukizwa homa ya Ebola.
Hii ni katika hali ambayo, watu 84 wamepoteza maisha nchini Ginea Conakry kutokana na kuambukizwa ugonjwa huo. Tayari Senagal imefunga mpaka wake na Guinea kwa hofu ya kusambaa virusi hivyo.
Shirika la Afya duniani limesema hali ya sasa ya ugonjwa huo imebadilika na kwamba virusi hivyo vina nguvu zaidi ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma. Dalili za homa ya Ebola ni kuhara na kutapika sambamba na joto kali mwilini ambalo pia huandamana na uvujaji mkubwa wa damu. Homa ya Ebola huambukizwa kwa kugusa damu, jasho na kinyesi cha mtu mwenye virusi hivyo.

0 comments: