Raia wasiopungua sita wa Misri wameuawa kwa kupigwa risasi na
askari usalama wa nchi hiyo katika maandamano yaliyofanyika jana mjini
Cairo kupinga serikali inayoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo.
Askari usalama wa Misri walikabiliana vikali na waandamanaji hao waliokuwa wakipinga mapinduzi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Mursi. Mwanafunzi kijana aliyekuwa na umri wa miaka 18 pia ni miongoni mwa watu waliouawa katika machafuko hayo huku madazeni ya wengine wakijeruhiwa.
Takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa serikali inayoungwa mkono na jeshi ya Cairo imewafunga jela raia elfu kumi na sita (16,000) tangu baada ya kuondolewa madarakani rais Muhammad Mursi Julai mwaka jana.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa pia limeeleza wasiwasi wake kuhusu mauaji na ukandamizaji mkubwa unaofanywa na askari usalama wa Misri dhidi ya raia wanaofanya maandamano ya amani wakiipinga serikali.

0 comments: