Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, yameonyesha kusikitishwa kwao kutokana na mauaji na ukatili unaofanywa dhidi ya Waislamu na waasi wa Kikristo wa Anti-Balaka nchini humo.
Ripoti iliyotolewa jana Jumatano na mashirika hayo imeeleza kuwa, sanjari na kupita mwaka mmoja wa mgogoro wa nchi hiyo, hali ya kibinadaamu inazidi kuwa mbaya na hivyo kutia wasi wasi siku hadi siku. Katika ripoti hiyo, jumuiya ya madaktari wasio na mpaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeonya dhidi ya ukatili na mauaji ya halaiki yanayofanywa dhidi ya Waislamu na kusisitiza kuwa, hali ya Waislamu nchini humo hivi sasa ni mbaya sana.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko tangu mwezi Machi mwaka jana, baada ya kupinduliwa madarakani na waasi wa muungano wa Seleka, aliyekuwa rais wa nchi hiyo François Bozizé, huku mauaji na ukatili wa kutisha dhidi ya jamii ya Waislamu, ukianza mnamo mwezi Disemba uliopita
0 comments: