Watu wasiojulikana wamewashambulia na kuwauwa viongozi wanane wa kikabila huko kusini magharibi mwa Somalia.
Ali Hassan kiongozi wa eneo la Buurhakabo lililoko katika jimbo la
Lower Shebelle kusini magharibi mwa Somalia amesema kuwa, viongozi hao wa kikabila wameuwa kwa kufyatuliwa risasi wakati walipokuwa wakielekea majumbani mwao.
Ali Hassan ameongeza kuwa, baada ya kutekelezwa mauaji hayo, kundi hilo la watu waliokuwa na silaha lilipora gari lililokuwa limewabeba viongozi hao.
Imeelezwa kuwa, viongozi hao wa kikabila hivi karibuni walishiriki kwenye uchaguzi ambao ulifanyika kwa lengo la kuainisha mpango wa kuundwa eneo litakalojitangazia mamlaka ya ndani na hatimaye kumteua Madoobe Nuunow, mmoja kati ya wababe wa kivita wa zamani wa Somalia, kuwa rais wa eneo hilo.
Hatua hiyo ya kuundwa eneo linalotaka kujitawala huko kusini magharibi mwa Somalia imekosolewa vikali na serikali kuu ya Somalia, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa
0 comments: