Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti nchini Uganda imefikia 108 baada ya wanamaji wa polisi ya Uganda kuopoa maiti 82 zaidi za wahanga wa ajali hiyo katika Ziwa Albert.
Polisi ya Uganda imesema boti hiyo ilikuwa na wakimbizi 150 wa Kikongo ambao walikuwa wakitoka katika kambi ya Kyangwali huko magharibi mwa Uganda.
Wakimbizi hao walikuwa njiani kurejea nchini kwao baada ya hali ya usalama kuimarika.
Jumapili iliyopita wavuvi katika Ziwa Albert walifanikiwa kuokoa abiria 45 waliokuwa ndani ya boti hiyo.
Uchunguzi wa awali unasema kuwa boti hiyo haikuwa na maboya ya kuokoa maisha na wala hapakupatikana msaada wa haraka wa kuokoa maisha ya watu waliofariki dunia.

0 comments: