Tuesday, June 21, 2016

Hivi kweli Rais Wetu Huguswi na Wabunge wa Upinzani Kutoka Bungeni?

at 9:57:00 AM  |  No comments

http://nicemediaworkstz.blogspot.com/
Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.

Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.

Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.

Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo. Mbona mwaka 1994 mwalimu aliingilia kati alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzisha serikali ya Tanganyika ndani muungano.

Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.