Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la
Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali
ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais.Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila
Bi. Ida Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry
Mulinganisa katika ibada ya pili ya pasaka Chato Mkoani Geita.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi.
Ida Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais
Dkt. John Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa
katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida
Odinga pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada
ya ibada.Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko
wa Parokia ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa .
Kikundi cha Kwaya ya vijana wakiimba katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amechangia kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia salamu zilizokuwa zikitolewa na Raila Odinga katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono kutakiana amani ya bwana na masista wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga wakiagana na waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sista Maria Theleza Ntihabose wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye yupo mapumzikoni nyumbani
kwake Lubambangwe katika kijijini cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita,
kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ameungana na waumini wenzake wa
Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato, kusali ibada ya Jumapili ya Pili ya
Pasaka ambapo pamoja na mambo mengine amewahusia watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa
na amani.
"Niwaombe
watanzania wote tuendelee kushirikiana na kushikamana, kwa umoja wetu na siku
zote tumtangilize Mungu mbele. Wakati tunaadhimisha wiki moja baada ya kufufuka
kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Yesu Kristo alikufa kwa sababu ya dhambi zetu, sisi
wote tujitahidi kufuata matendo ya Yesu Kristo ya kusameheana, kupendana,
kushirikiana na tusibaguane" Amebainisha
Rais Magufuli.
Pamoja na Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, ambao ni
familia rafiki wa Rais Magufuli, waliowasili hapa Chato jana jioni Tarehe 02
April, 2016 kwa mapumziko wakitokea Nairobi, Kenya.
Katika salamu zake
kwa waumini wa Parokia ya Chato, Mheshimiwa Odinga amewashukuru watanzania kwa
uhusiano mzuri walionao na wakenya, huku akitoa mfano wa jinsi Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyojitoa kupigania uhuru wa mataifa mengi
ya Afrika ikiwemo Kenya.
Mheshimiwa Odinga
ametoa mfano wake mwenyewe kuwa Mwalimu Nyerere alimpatia pasi ya kusafiria ya
Tanzania, aliyoitumia kwa miaka mitatu kwa ajili ya kwenda kusoma nje ya nchi,
baada ya utawala wa Kikoloni wa Kenya kukataa kumpa pasi hiyo.
Kuhusu urafiki
wake na Rais Magufuli, Mheshimiwa Odinga amesema urafiki huo ulianza tangu Rais
Magufuli alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na yeye kuwa Waziri mwenye dhamana
ya ujenzi wa Kenya, ambapo mara kadhaa walibadilishana uzoefu na kushirikiana
katika mipango ya miradi ya ujenzi wa barabara, na kwa umuhimu huo ametoa wito
kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano na mshikamano
ulioasisiwa na waasisi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Jalamogi
Odinga wa Kenya na Milton Obote wa Uganda.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
0 comments: