Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kutembelea shule ya msingi Nzuguni
B. Kulia kwake ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki
Jaffari Mwanyemba aliyeongozana na Mhe. Naibu waziri katika ziara hiyo.
Na Rebecca Kwandu
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa
na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi mara kwa mara ili kujionea
hali halisi na kutatua kero zilizopo.
Akizungumza
na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B. wakati wa ziara aliyoifanya
kutembelea shule hiyo na shule ya sekondari Nzuguni A., Mhe. Jafo
alisema watumishi hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo watakuwa
hawatembelei na kukagua maeneo yao ya kazi.
“
Kumekuwa na uzembe kwa Wakuu wa Idara kutokusikiliza matatizo ya chini,
kutowatembelea watumishi waliopo chini yetu inawasababishia kukosa
mahali pa kusemea shida zao na kuchanganyikiwa. Ni vizuri kuwa na
utaratibu wa kuwatembelea watumishi tunaowaongoza ili kujua shida zao na
kuzitatua. Alisisitiza Mhe. Jafo.
Aidha,
aliwataka walimu wa shule za msingi Nzuguni B na Shule ya sekondari
Nzuguni A kuweka utaratibu wa kuweka malengo na kujipima kuona
walichokifanya ili kupata matokeo tarajiwa.
Wakati
huo huo, Naibu Waziri wa Nchi Jafo ametoa Mabati 164 ili kuchangia
ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Nzuguni B iliyopo kata ya Nzuguni
katika halmashauri ya Mji wa Dodoma.
Mhe.
Jafo alitoa Mabati hayo baada ya kufanya ziara ya kutembelea shule hiyo
ili kujionea hali halisi ya maendeleo yake ikiwa ni moja ya taratibu
alizojiwekea za kutembelea maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Ofisi ya
Rais-TAMISEMI ili kujionea changamoto mbalimbali zilizopo katika utoaji
wa huduma na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
ziara hiyo Mhe. Jafo alikuta Idadi kubwa ya watoto walioandikishwa
kujiunga na darasa la kwanza hali iliyopelekea kukosekana kwa vyumba
vya kutosha kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi ambapo kwa kutatua kero
hiyo, shule hiyo imeanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwa upande
wake alichangia bati 164 ili kuwezesha madarasa hayo kukamilika.
0 comments: