Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia
mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa madarasa
wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono jitihada za
Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani ya Shs.
7,000,000/= yalikabidhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel
Kyungu akikagua mabati yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF
wilayani Geita, kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine
ni maofisa kutoka wilaya ya Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shikrani kwa Mfuko
wa Pensheni LAPF kwa msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita
(6) vya madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo
kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF James Mlowe pamoja na wafanyakazi mbalimbali wa Wilaya ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
0 comments: