Katibu
Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya
ya Chalinze. Tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia nyaraka za gari hilo
la kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari la
kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es
Salaam.
0 comments: