Friday, March 18, 2016

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA NHC.

at 11:15:00 AM  |  No comments

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha NHC.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo.

Share
, Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.