Mwenyekiti
wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk.
Rehema Laiti cheti cha shukrani kwa kumaliza shahada ya uzamili katika
matibabu ya saratani ya watoto na kwa mchango mkubwa katika kuokoa
maisha ya watoto. Katikati ni Dk. Trish Scanlan, Mwanzilishi wa Asasi ya
Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk.
Shakilu Jumanne cheti cha shukrani kwa kumaliza shahada ya uzamili
katika matibabu ya saratani ya watoto kwa mchango mkubwa katika kuokoa
maisha ya watoto. Katikati ni Dk. Trish Scanlan, Mwanzilishi wa Asasi ya
Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk.
Moses Karashani cheti cha shukrani kwa mchango mkubwa katika kuokoa
maisha ya watoto wenye saratani. Katikati ni Dk. Trish Scanlan,
Mwanzilishi wa Asasi ya Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akiwa kwenye
picha ya pamoja na madaktari Moses Karashani aliyepewa nafasi ya kusoma
uzamili wa kutibu saratani kwa watoto (kushoto) na Dk. Rehema Laitu (wa
pili kushoto) na Dk. Shakilu Jumanne ambao walipatiwa vyeti vya shukrani
kutokana na ubobezi katika matibabu ya saratani ya watoto.
(Picha: Mpiga Picha Wetu)
TAASISI
ya Karimjee Jivanjee imetoa nafasi za masomo kwa madaktari watatu wa
Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wake kuwajengea uwezo madaktari wa
Tanzania ili waweze kuwa wabobezi katika matibabu ya saratani kwa
watoto.
Madaktari
hao wamepewa fursa za kusomea shahada mpya ya uzamili katika matibabu
ya saratani kwa watoto wadogo inayotolewa na Chuo Kikuu cha Tiba
Muhimbili. Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, amesema jijini
Dar es salam leo kwamba taasisi hiyo inataka kuweka mazingira endelevu
katika ubora wa huduma za afya kwa kuwajengea uwezo madaktari kuweza
kuwatibu watoto wadogo wenye ugonjwa wa saratani.
“Ili
kutimiza lengo hili ni lazima wapatikane madaktari wenye sifa nchi
nzima,” alisema Karimjee wakati akiongea kwenye hafla ya kuwapongeza
madaktari waliomaliza kozi hiyo mwaka 2015 na wanaoanza kozi ya 2016
chini ya udhamini wa Karimjee Jivanjee Foundation.
“Mwaka
2014, Tanzania haikuwa hata na daktari mmoja wa mwenye sifa za kutibu
saratani kwa watoto lakini baada ya Daktari Trish Scanlan pamoja na
Taasisi ya Tumaini la Maisha kuanzisha kozi hiyo ya uzamili kwa
ushirikiano na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, taasisi ya Karimjee iliona
kwamba ni muda muafaka kutoa mafunzo kwa madaktari wa Kitanzania katika
eneo hili na ndio maana tuliamua kusaidia program hii.”
Mwaka
2014 tulitoa nafasi za masomo kwa madaktari wawili kusomea kozi hiyo
mpya na pamoja na mafunzo ya miezi mitatu nchini Ireland ili kupata
uzoefu wa kimataifa ambapo kozi nzima iligharimu shilingi milioni 70.
Madaktari walionufaika na program hiyo ni Dokta Rehema Laiti na Dk.
Shakilu Jumanne ambao wamemaliza masomo na mafunzo yao na sasa
wameajiriwa na Hospitali ya Taif ya Muhimbili kwenye kitengo cha
saratani kwa watoto.
Katika
hafla hiyo, taasisi za Karimjee na Tumaini la Maisha waliwapatia
madaktari hao vyeti vya shukrani kwa kazi wanayofanya kuokoa maisha ya
watoto. Madaktari hao pia walizawadiwa shilingi milioni 6.6 kila mmoja
ili waweze kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu watoto wenye kansa
litakalofanyika Dublin nchini Ireland Oktoba mwaka huu 2016. Taasisi ya
Karimjee Jivanjee pia ilimtangaza Dokta Moses Karashani kuwa daktari
atakayenufaika na programu hii kwa mwaka 2016.
0 comments: