Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni
10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi
kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu
na kiongozi huyo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya
saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya
saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa
mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.
Mkuu
huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na
watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya
simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya
hivi karibuni.
Msaidizi
wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka
atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya
kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua
kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa
Wilaya.
Kwa
upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini
alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.
Wizi
wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho
teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za
kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa
kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo
Na udaku Special
0 comments: