Msafara wa Pikipiki ukimsindikiza mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na UKAWA ,James Mbatia wakati wa kwenda kufanya uzinduzi wa Kampeni katika jimbo jilo. |
Msululu wa magari ukimsindikiza mgombea huyo. |
Maeneo mbalimbali aliyopita mgombea huyo alipokelewa na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wamesimama kando ya barabara wengi wao wakiwa ni kina mama. |
Katika maeneo mengine wananchi walisimamisha msafara wake na kusalimia kwa muda kabla ya kuendelea na safari. |
Shughuli zilisimama kwa muda katika maeneo mbalimbali angalau kutoa nafasi japo kupunga mkono kwa mgombea huyo. |
Msafara ukielekea uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ualimu cha Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa mkutano wa Kampeni. |
Makondakta na madereva wa daladala katika eneo la Marangu mtoni wakisalimiana na mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo ,James Mbatia. |
Hii ndivyo ilivyokuwakatika eneo la Marangu Mtoni. |
Raia wa kigeni wakichukua taswira za mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo,Jmaes Mbatia. |
0 comments: