NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Monday, June 22, 2015
MAFUNZO YA UONGOZI WA MAGEREZA DARAJA LA PILI JIJINI DAR ES SALAAM YAFUNGWA RASMI NA IGP MANGU..Tazama hapa..
at 11:50:00 PM | 
No comments
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo.
Maafisa wa Jeshi la Magereza wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu mbalimbali za kujihami na adui kama wanavyoonekana kikakamavu katika picha wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza.
Kikundi cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambayo yamefungwa rasmi leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya Mgeni rasmi IGP Ernest Mangu(hayupo pichani) katika mwendo wa haraka wakitoa heshima leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216 wamehitimu Mafunzo
Uongozi Daraja la Pili na kupandishwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(kushoto katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akifurahia onesho Maalum la Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile wakifurahia onesho hilo kama wanavyoonekana katika picha.
Share
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
UMEIPATA HII..JAMAA ALA KICHAPO BAADA YA KUHISIWA NA WANACHAMA KWENYE MKUTANO WA UKAWA..Ingia hapa..
NICE STUDIO YA JIJINI ARUSHA YAPANIA KUWAINUA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI.Tazama hapa.....
SERIKALI NA TTCL KUMILIKI KWA PAMOJA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO.
WATU MAARUFU WA WAFIKA KUUAGA MWILI WA KAPTENI JOHN KOMBA HAKIKA ALIKUWA MTU WA WATU...Tazama hapa
UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI..UNGO HUU UNATUMIKA KUANGALIA MPIRA LIVE KUTOKA BRAZIL..Tazama hapa..
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: