Mwenyekiti
wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald
Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao
ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey
Mpandikizi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza
katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers
na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald
Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu
nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya
habari.
Wadau na wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari na wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI
wa Vyombo vya habari nchini (MOAT) wameitaka serikali kutosaini muswada
wa vyombo vya habari kutokana na kutokuwa wa haki na kwamba unavibana
vyombo vya habari.
Pia
wamiliki hao wamesema kama serikali inataka kuupitisha isubiri Rais
ajaye ndiyo aupitishe wakati huohuo wameunda kamati maalumu itakayoenda
Mjini Dodoma kuuzuia usipitishwe wala kujadiliwa bungeni.
Akizungumza
Dar es Salaam leo mchana Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (MOAT), ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni
ya IPP, Regnald Mengi alisema anashangazwa sana na wanasisa kusahau
walipotoka kutokana na kusapoti muswada huo kupitishwa.
Alisema
serikali imeamua kufanya hivyo kutokana na kusahau waliowasababishia
kupata madaraka kutokana na shida yao kuisha hivyo vyomba vya habari
vimejifunza.
"Tumejifunza
kuwa sisi ni8 watu wa kutumika wanapotaka kututumia hivyo wanataka
kutumaliza na muswada huu hivyo sioni kama wana nia njema na sisi,
"Alisema Mengi.
Aliongeza
nia ya kupitishwa kwa muswada huo so njema na kwamba haki ya kupata
habari sio tuu haki ya msingio bali ni ya kikatiba hivyo serikali isije
ikajihusiasha na kuvunja katiba ya nchi bali inatakiwa kuonesha mfano
bora.
Akizungumzia
kuhusu Demokrasia alisema mtu hawezi kufanya vitu visivyozingatia
demokrasia ili kudhibiti demokrasia au kuhakikisha unapata demokrasia
kwa kutumia njia za kidemopkrasia bali anapaswa kutumia amani.
"Huwezio
kuheshimu sheria kwa kutumia nguvu, hivyo muswada ukiwa na sheria onevu
na isiyokubalika au kukiuka katiba ya nchi lazima hali itakuwa mbaya
nchini,"
Kwa
upande wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu alisema watanzania tunaelekea
kwenye mchakato huo lakini hatuwezi kuwa na uchaguzi huru ikiwa vyombo
vya habari havina uhuru wa kupokea na kuandika habari ili watanzania
waweze kuelewa hivyo serikali inatakiwa kujadili kwa makini ili kunusuru
machafuko yanayoweza kujitokeza.
"Hatuwezi
kuficha vitu wakati mambo yanatakiwa yawe wazi, na kama tungekuwa
tunataka uwazi tusingeruhusu vyombo vya habari kuwa wazi, hivyo muswada
huo utatupa matatizo kwenye uchaguzi na hauwezi kluwa huru pasipo
wananchi kujua nuini kinaendelea kupitia vyombo hivyo,"alisema Mengi.
Hata
hivyo mengi aliongeza kuwa hakuna amani endelevu bila kuwepo uhuru na
haki kwa kuwa ni rasilimali kubwa ya taifa na kwamba si ya mtu mmoja,
kikundi wala chama bali ni yetu sote hivyo serikali ikijaribu kuichezea
itakuwa inacjhezea wananchi wa tanzania.span>
Kwa
upande wake Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Godfrey Mpandikizi akizungumzia changamoto zilizopo kwenye muswada
huo,alisema vitu vilivyopo kwenye muswada huo vinakinzana na katiba ya
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hivyo aliwataka wahariri kwenda Dodoma
kuuzuia.
Alisema
muswada huo pia unazuia jamii kujua mambo yanayoendelea hivyo
itasababisha hali ya nchi kuwa mbaya kwa siku zijazo kurtokana na kuwa
na mapungufu zaidi ya 10 katika kila kifungu pamoja na tafsiri zaidi ya
20.
"Sheria
hiyo ni chafu, na hairuhusiwi kwenda bungeni hivyo isubiri Rais ajaye
na katiba mpya ndiyo ujadiliwe ili uwe na haki hivyo wamiliki nendeni
Dodoma mkauzuie usijadiliwe na wabunge waka kupitishwa,"alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai aliwataka wamiliki
hao kuonana na wanasheria, wabunge na mashirika mengine kwenda mahakani
kupinga sheria hiyo chafu.
0 comments: