Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmojawa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi
wengine sita kuanzia jana, Jumamosi,Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili,Desemba 7, 2014 na Katibu MkuuKiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefuemjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais
amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu,
Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi FelixNtibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho,Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne
asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu
waliohamishwa vituo vya kazi niMheshimiwa Elaston Mbwiloanayehamishwa kutoka Mkoa waManyara kwenda Mkoa wa Simiyu
ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa
likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa
wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M
Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa
Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza
anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa
Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka
Mkoa wa Arusha.Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo
vyao vya sasa vya kazi Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam
6 Desemba, 2014
0 comments: