Wednesday, March 19, 2014

Wakati Tanzania wakijadili rasim ya katiba mpya Wapinzani wa Kongo wapinga marekebisho ya katiba

at 3:27:00 AM  |  No comments

     Wapinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamepinga azma ya chama tawala ya kuifanyika katiba merekebisho. Hayo yamejiri baada ya wafuasi wa Rais Joseph Kabila kutaka kuifanyia marekebisho katiba ili kumuandalia rais huyo mazingira ya kugombea tena katika uchaguzi ujao suala ambalo limezusha mjadala mkubwa nchini humo.

Chama tawala cha Kongo kwa kufuata mfano wa katiba ya Afrika Kusini kinakusudia kufanyia marekebisho kipengee nambari 220, ili kumuwezesha rais wa nchi kubakia madarakani kwa vipindi vitatu. Wapinzani wanasema nia hiyo ni kama 'kulipua bomu' nchini.

 Kiongozi wa wawakilishi wa upinzani bungeni Martin Fayulu amesema kuwa, uamuzi huo unakinzana na katiba yenyewe kwani kwa mujibu wa katiba kila mtu anaweza kuongoza nchi kwa vipindi viwili tu. Rais Kabila tayari ameiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa vipindi viwili, muda utakaomalizika kwa kuitishwa uchaguzi mpya ifikapo mwaka 2016.

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.