Tuesday, October 7, 2014

WASSIRA AFANYA KWELI KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA JONH LISSU DIAMOND JUBILEE

at 1:39:00 AM  |  No comments

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira akikata utepe wakati wa uzinduzi wa album ya nyimbo za injili ya ‘Uko Hapa’ yenye nyimbo 18 ya mwimbaji,  John Lisu wakati wa uzinduzi wa album hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, mwishoni wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni mdhamini wa uzinduzi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira akionyesha album ya  ‘Uko
Hapa’ yenye nyimbo 18 ya mwimbaji,  John
Lisu wakati wa uzinduzi wa album hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam, mwishoni wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni mdhamini wa uzinduzi huo.
 John Lisu akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa Album yake ya ‘Uko Hapa’
Mary Lisu (kushoto), akiimba sambamba na John Lisu wimbo mpya ujulikanao kwa jina la Mfalme ambao Albam yake iko jikoni wakati wa uzinduzi wa Album ya John Lisu ya ‘Uko Hapa’ uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Waimbaji wa John Lisu wakiwajibika jukwaani wakati wa uzinduzi wa Album ya ‘Uko Hapa’.
Mary Lisu akiimba wimbo wa mpya ujulikanao kwa jina la Mfalme ambao Albam yake iko jikoni wakati wa uzinduzi wa Album ya John Lisu ya ‘Uko Hapa’ uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
 ………………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu
 
MWIMBAJI  nguli wa muziki wa Injili Tanzania, John Lisu juzi
alikonga nyoyo za mamia ya wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa albamu yake
ya Uko Hapa yenye nyimbo 18, uliofanyika katika Diamond Jubilee, jijini Dar es
Salaam.
 
Uzinduzi huo uliofanyika mbele
ya mgeni rasmi, Waziri wa Waziri Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephn
Wassira, ulikuwa na mvuto mkubwa sio tu kutokana na umahiri wa mwimbaji huyo,
pia maandalizi yaliyofanywa na wadhamini.
 
Lisu alipopanda jukwaani,
alifanya kweli kwa kuimba nyimbo zaidi ya tano zilizopo katika albamu hiyo
iliyozinduliwa.
 
Lisu aliyepanda jukwaani
saa 12 jioni, alidhihirisha uwezo wake wa kushambulia jukwaa kwa kuimba hadi
saa mbili bila kuonesha kuchoka.
 
Uzinduzi wa albamu hiyo
uliofanywa na  Waziri Wasira, iliwekwa
baraka baada ya kuzinduliwa na maaskofu watano
wa Makanisa tofauti.
 
Hao ni Askofu Lawrance
Kametta (TAG-Jimbo la Mashariki), Askofu Deo Rubala (Word Alive Centre), Askofu
Bruno Mwakibolwa, Mtume Peter Nyaga (RGC-Miracle Centre) na Machungaji Paul
Safari (DPC).
 
Lisu alilitumia jukwaa
hilo lililolipuka kwa shangwe za mashabiki alipoimba na mkewe, Nelly wimbo wake
mpya wa Mfalme ambao unatarajia kuwemo katika albamu yake mpya ambayo ipo
katika maandalizi.
 
Aidha, Lisu kabla ya
kuimba na mke wake (Nelly), alitumia jukwaa hilo kuwatambulisha watoto wake
mapacha na kuwabariki ambako pia alitoa ushuhuda baadaye watakuwa wachungaji.
 
Pia, jukwaani aliimba
mojawapo ya nyimbo zake na muimbaji kutoka Kenya, Timoth Kaberia.
Aidha, Lisu alitumia
fursa hito kutoa shukrani kwa waliofanikisha safari yake ya muziki huo. 
 
DVD hizo zilizozinduliwa
ambazo idadi yake ni 18 zimegawanyika sehemu mbili ni pamoja na Wakusifiwa,
Wastahili sifa, uko juu, Inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili Bwana,
Roho Mtakatifu na Mtakatifu.
 
Nyingine ni Yu Hai
Jehovah, Atikisa, Upendo Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua
Macho, Haleluya na Mungu Ibariki.
 
 Naye Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni
wadhamini wa uzinduzi huo, Alex Msama, alishukuru mapendekezo ya mabadiliko
yaliyopendekezwa katika Katiba mpya ambayo yanawatambua wasanii.

Alisema kutambulika huko
kumetokana na mshikamano uliopo katika ya wasanii na serikali hivyo alitoa wito
kwa wasanii kuongeza jitihada za ufanikishaji wa kazi zao.

Share
, , Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.