Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati (kushoto), akikata utepe kuashiria makabidhiano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo wa trekta, Mkulima Karoli Lubuva katika hafla hiyo. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni wakulima kutoka Kwadelo mkoani Dodoma.Na Mwandishi wetuKAMPUNI ya Kariati Trekta imewakabidhi matrekta manne yenye thamani ya sh.milioni 100 kwa wakulima kutoka mkoani Mbeya na wilayani Kondoa baada ya kuwakopesha kwa bei nafuu.Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi matrekta hayo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati alisema matrekta hayo yatawasaidia katika kilimo ambacho kitawainua kiuchumi.Alisema kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka miwili imewakopesha wakulima zaidi ya matrekta 84 ambapo kila anayekopa anatakiwa sh.milioni 25 kwa awamu mbili."Kila mkulima anaye kopeshwa kwa awamu ya kwanza anatakiwa kutoa sh.milioni 18 na baadae anamalizia kiasi kilichobaki" alisema Kariati.Alisema kampuni yake hiyo imelenga kuwasaidia wakulima kuepukana na jembe la mkono na linatoa mkopo huo kwa mkulima yeyote ndani ya Tanzania.Kariati alitoa mwito kwa wakulima kutumia fursa hiyo ya kukopa matrektra hayo ili kujikomboa kiuchumi na kustawisha maisha yao na kuondokana na umaskini.
0 comments: