Mtu mmoja amefariki Mkoani Iringa baada ya lori lililobeba mafuta kupinduka na kuteketea kwa moto kisha kusababisha majeruhi kwa mmoja
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP. Ramadhani Mungi amemtaja marehemu kuwa ni Tony Shilla mkazi wa mkoani Mbeya ambaye amefariki papo hapo kwa ajali ya moto huo.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa Brayton Mwambongika umri wa miaka 34 dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 198 CZS aina ya Scania amejeruhiwa ambapo amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa akiendelea na matibabu zaidi.
Hata hivyo Kamanda Mungia meongeza kuwa ajari imetokea maeneo ya Igeme, tarafa ya Mahenge, wilayani Kilolo, mkoani Iringa na jeshi la polisi Mkoani Iringa linaendelea na kufanya uchunguzi zaidi wa kubaini chanzo cha ajali hiyo
0 comments: