Afisa Habari wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa TMAA kwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) wakati alipotembelea kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya MnaziMmoja, jijini Dar es Salaam.
Mashine ya kisasa ya kupimia ubora wa sampuli za madini ikioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao. Wanaomsikiliza ni Afisa Habari, Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) na Afisa Utumishi, Bibi Fatma Chondo (Katikati).
0 comments: