WAANDISHI
wa Habari mkoani Singida, wamehimizwa kuondokana na uandishi habari wa
mazoea na badala yake wabadilike na kuwa wabunifu ili kazi yao iweze
kukidhi viwango vya wakati uliopo. Changamoto hiyo imetolewa hivi
karibuni na mwandishi wa habari mkongwe, Eda Sanga wakati akizungmza
kwenye semina ya Uhabarisho wa Mfuko wa Habari Tanzania (Tanzania Media
Fund TMF) kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida. Amesema waandishi wa
habari ule wa business as usual, haufai umepitwa na wakati unadumaza
maendeleo ya mhusika. amesema uandishi wa habari kwa sasa umetakiwa
mwandishi wa habari ujitume, uwe mbunifu, ufanye uchunguzi wa kina ili
ukiandika habari watu wakupongeze au wakusifu.
“Ninyi mnapaswa katika kutekeleza majukumu yenu muiangalie Singida kwa upana wake. Ni kero gani zinawasibu wananchi. Nini kifanyike ii kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kero hizo” Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida,wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na maafisa kutoka Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) juu ya kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na mfuko huo.Picha na Nathaniel Limu.
Afisa kutoka Mfuko wa Waandishi wa Habari Tanzania (TMF) Alex Kanyambo akitoa mada yake juu ya umuhimu wa vilabu vya waandishi wa habari kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na TMF.Wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa TMF,Japhet Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Seif Takaza. Kwa hali hiyo, aliwataka kujitathimini juu ya utendaji wao wa kila siku na wahakikishe habari zao zisiwe na upande moja mbali ziwe ‘balanced’.
Mwandishi wa habari mkongwe nchini,Eda Sanga akizungumza kwenye semina ya uhabarisho juu ya shughuli za Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyohudhuriwa na waandishi wa habari mkoa wa Singida. Awali Afisa Habari wa TMF makao makuu,Japhet Sanga amewahimiza waandishi wa habari nchini kujenga utamaduni wa kuomba uwezeshaji wa fedha kutoka TMF ili pamoja na mambo mengine kuongeza uzoefu zaidi katika kutekeleza majukumu yao. Akifafanua, amesema TMF inatoa ruzuku ya fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi ambazo zinaibua mambo mengi mapya na hasa kero zinazowakabili wananchi wakiwemo wa vijijini. “TMF tunaamini kwamba kwa vyo vyote habari za uchuguzi zitamwezesha mwandishi husika kujifunza mambo mapya kwa hiyo atakuwa amepanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi”.,amesema

0 comments: