Wednesday, May 7, 2014

MKUU WA MAJESHI AKWEPA KUZUNGUMZIA KAULI ZA WANASIASA JUU YA JESHI KUPINDUA NCHI

at 4:51:00 AM  |  No comments

 http://themonthlyjob.com/?refcode=7863
Arusha,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange,juzi  amekwepa kuzungumzia au kutoa ufafanuzi kuhusu kauli zinazotolewana baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwa iwapo muundo wa serikali tatu utapitishwa,Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa Tanzania (JWTZ) linaweza kupindua nchini.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano mkuuwa nane wa Wakuu wa Idara za Ukaguzi za Majeshi (DIWG) kutoka nchi zaJumuiya ya Maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC), Jenerali Mwanyange,alisema hawezi kujiingiza katika masuala ya siasa.Alitoa jibu hilo kufuatia swali aliloulizwa na mwandishi kuhusu anakauli kauli gani kufuatia baadhi ya viongozi kulihusisha jeshihilo na siasa .“Siwezi kujibu hilo swali, siwezi kujiingiza katika haya masuala. ni sawa mimi mchezaji wa mpira wa miguu uniulize swali kuhusu mpira watennis” alisema na kusisitiza aulizwe kuhusiana na mkutano unaoendelea.
Baadhi ya wanasiasa, wamekuwa wakitoa kauli, katika bunge maalum la Katiba kuwa, kama muundo wa Serikali tatu, ukipita wataingia msituni na wengine wakisema jeshi linaweza kupindua nchi kwani serikali ya Muungano inayopendekezwa katika rasimu ya Katiba, itakuwa na jukumu la kulipa mishahara ya majeshi lakini haina mapato ya uhakika.Mapema akifungua mkutano huo jijini hapa jana, Jenerali Mwamunyange,aliwataka wakuu wa idara za ukaguzi katika majeshi ya SADC,kuhakikisha majeshi yao yanakuwa tayari wakati wowote kutekelezamajukumu yao.Alisema ukaguzi wa majeshi ni jambo muhimu ili kujua iwapo yapo tayarikutekeleza majukumu yao katika kulinda amani, usalama wa mipaka yanchi wanawachama. Akizungumzia mkutano huo, Mwenyekiti wa(DIWG) BornwellNjilika  alisema  chombo hicho cha wakaguzi wa majeshi kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwepo upungufu wa fedha  na uchache wa watumishi wa makao makuu waliopo Botswana.Katika mkutano huo, Tanzania iliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa DIWG chini yaBrigedia Jenerali Emmanuel Edward Maganga.

Share
Posted by Unknown
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

Text Widget

Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.