Ni mwaka mmoja, tokea Rais Kenyatta aapishwe kuanza kulitumikia taifa la Kenya .
Alitoa ahadi nyingi; ikiwa pamoja na kuuendeleza uchumi, kuuimarisha
umoja wa taifa na kuweka utaratibu wa huduma za afya zinazoweza kulipiwa
na kila mwananchi .Rais Kenyatta pia aliahidi kuleta uhakika wa
chakula, kutenga nafasi za ajira kwa vijana na kugawa "Laptop" kwa
watoto wote wa shule za msingi.Lakini aliyoweza kuyafanya ili
kuzitekeleza ahadi hizo ni machache hadi sasa.
Bei za vyakula zimezidi kupanda, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana
bado ni wa kiwango cha juu na hasa katika sehemu za mashambani .Aidha
mpango wa kugawa "Laptop" kwa watoto wa shule umesahauliwa ndani ya
mtoto wa meza kufuatia kashfa.
Mwandishi habari mmoja Inchikirwa Ndelejai amesema serikali ya Kenyatta
haijafanya mengi. Amesema serika ya mfungamano wa Jubilee haijafanya ya
kutosha. Ameeleza kwamba serikali haikufanya kama ilivyoahidi.
Mwandishsi habari huyo amesema ,ikiwa mtu atawapima wanasiasaa katika
msingi wa ahadi walizozitoa, basi kilichofanyika hadi sasa ni cha
kusikitisha.
Hatua fulani zapigwa
Hata hivyo hatua kadhaa zimepigwa na serikali ya Kenyatta katika kuzitekeleza baadhi ya ahadi.
Mara tu baada ya kuchaguliwa Kenyatta alianza kuutekeleza utaratibu wa
kutoa huduma kwa ajili ya wajawazito bila ya malipo.Akina mama hawalipii
gharama za kupimwa wanapokuwa wajawazito na pia hawalipii gharama za
kujifungua.Katika hotuba yake Rais Kenyatta ,alisifu mafanikio
yaliyopatikana katika uchumi na hatua zilizochukuliwa katika kupambana
na ufisadi.
Hatua fupi katika kupambana na ufisadi
Hata hivyo kuhusu ufisadi ndani ya polisi,mwakilishi wa Wakfu Ujerumani
wa " Heinrich Böll" nchini Kenya Katrin Seidel amesema kwamba maafisa
wengi wa polisi waliohusika na vitendo vya ufisadi vilivyoweza
kuthibitishwa bado wanaendelea na kazi na bado wamo katika ngazi za
uongozi pia katika idara ya usalama. Mwakilishi huyo wa Wakfu wa
Ujerumani ,bibi Seidel amesema watu wengi nchini Kenya wanahisi kwamba
hawahudumiwi kwa kiwango cha kutosha katika suala la usalama.
Kutokana na shambulio la magaidi kwenye jengo la maduka,Westgate mjini
Nairobi mwezi Septemba mwaka uliopita Wakenya wengi wamepoteza imani juu
ya idara za usalama. Lakini juu ya suala la usalama Rais Uhuru Kenyatta
amesema " usalama wa watu wetu na ulinzi wa mipaka ya nchi ni miongomi
mwa wajibu wangu mkuu." Rais Kenyatta amesema vitisho vyovyote dhidi ya
mipaka ya Kenya vitakabiliwa kwa uwezo na nguvu zote za watu wa Kenya.
Umaarufu wa Kenyatta katika utaifa
Katika upande mwingine Rais Kenyatta anatumia turufu ya utaifa ili
kuhakikisha umaarufu wake. Hata kesi inayomkabili kwenye Mahakama Kuu ya
Kimataifa ya ICC inapalilia umaarufu wake.
Rais Kenyatta anakabiliwa mashkata ya uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ghasia zilizotokea nchini Kenya kufuatia uchaguzi wa Rais mnamo mwaka wa 2007 inadaiwa kuwa Kenyatta ambae wakati huo alikuwa kiongozi wa chama ndiye aliehamamisha makundi yaliyowatimua watu wa makabila mengine,yaliyofanya ubakaji na kuwaandama watu wa jamii nyingine.
Wednesday, April 9, 2014
Rais Uhuru Kenyatta atimiza mwaka mmoja madarakani.Ni nini Amefanya? Soma hapa,.
at 4:22:00 AM |  No comments
Share
MATUKIOPosted by Unknown
- HII NI AJALI MBAYA SANA ILIYOHUSISHA MABASI 2 KUGONGANA USO KWA USO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 30 PAPOHAPO..Samahani kwa picha
- KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA KUNA VITUKO...Hivi ndivyo ilivyokuwa Bofya hapa ujioneeeee
- Mkutano wa Ulaya na Afrika waanza Brussels
- MWIGULU NCHEMBA AANZA SAFARI YA KUHAKIKISHA WAFUGAJI WANAACHA KUFUGA KIHOLELA,WAFUGE KWA VITALU.
- Tazama HIVI NDIVYO MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YALIVYOFANA....Bofya hapa.....
0 comments: