Sasa wanaiomba serikali kuboresha huduma zake za kijasusi ili kuwawezesha kukabili ugaidi ama uhalifu wa aina yoyote.
Na kama anavyoripoti Ronald Mutie kutoka mji mkuu Nairobi, serikali pia inatoa onyo kali kwa wale wanaochochea mauaji haswa kupitia kwa dini mbalimbali.
Watu wanaendelea na shughuli zao za kila siku katika mji Nairobi .
Katika duka moja ni wakaazi wakinunua bidha……. na kwenye kanisa mahubiri ya saa saba yanaendelea.
Lakini licha ya hali ya utulivu na mazingira ya amani wakaazi wana wasiwasi.
Shambulizi la jumapili wiki jana kwenye kanisa moja Mjini Mombasa Pwani ya kenya ni jambo la kutia hofu kwao.
"Ukienda kanisani una wasi wasi na wale wanaenda msikitini pia wana wasi wasi wanaweza kushambuliwa wakati wowote"
"Sijaamini kwamba niko salama …usalama ni wa hali ya chini"
Nchini Kenya askari mmoja anawalinda watu 600 hii ikiwa ni chini ya kiwango cha kimataifa cha polisi 300 kwa watu elfu mia moja.
Idadi hii ndogo ya polisi pia inakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kutekeleza shughuli za usalama.
Wananchi wanaona serikali inafaa kuboresha uwezo wa polsi wa kulinda usalama kwa kuwa na vifaa na mipango mwafaka.
Na wanaiomba kuongeza juhudi za jijasusi na kuimarisha usalama wa taifa.
"Serikali inunue vyombo na kuwapea askari ili kuwasaidia kutekeleza kazi zao"
"Askari wanafanya kazi lakini hawana vyombo vya kuwawezesha kufanya kazi ipasavyo. Kwanza wawekeze katika ule msingi wa kukusanya habari kuhusu usalama na kuzifuatilia"
Lakini wakati wananchi wakiomba kuboreshwa kwa huduma za polisi mtaalamu wa masuala ya usalama Bw.Gideon Maina anasema pia wao wenyewe wana jukumu la kulinda usalama.
"Jukumu la usalam wan chi sio la polisi lakini ni la mwananchi.kama nchi ni lazima tuweke mikakati kabambe ili tupambane na ugaidi"
Tangu kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia mwaka wa 2010 Kenya imekuwa ikishuudia mashambulzi katika maeneo mbali mbali na zaidi ya watu 200 wameuwawa kulingana na taakwimu za polisi.
Wataalam wanasema mengi ya mashambulizi yanatekelezwa na wafuasi wa kundi la Al shabaab ambalo linapinga serikali nchini Somalia.
Hata hivyo Serikali ya kenya imehapa kuendelea na oparesheni zake dhidi ya Al-shabaab kwani kundi hilo lilikuwa linashambulia na kuteka watalii kutoka Kenya.
Aidha imeanzisha mipango kadhaa ya kuimarisha usalama mipakani na ndani ya nchi.
Lakini kuna changamoto.
Baadhi ya viongozi wa kidini kama Hilunga Hassan wamelaumiwa kwa kuhubiri itikadi zinazochochea mauaji.
Akiuwawa Shekhe mtafute padri muuwe"
Matamshi yake hayo yamekashifiwa na Rais Uhuru Kenyatta na kukariri kwamba dini haiwezi kutumika kama chombo cha kueneza kampeni za mauaji.
"Kwa wale wachache ambao wanafikiria watatumia dini kuuwa wakenya wenzao tunasema sio katika taifa la Kenya"
Kama njia moja ya kukuza usalama wa kiraia mwaka jana serikali ilisema itaanza mpamgo wa nyumba kumi utakaowezesha kilamkenya kumjua vyema jirani yake.
Lakini ijapokuwa mpango huo haujatekelezwa huenda ukasaidia kupunguza visa vya ukosefu wa usalama nchini, pale utakapoanza.
0 comments: