Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
itatoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123
wanaosafirisha Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na
matumizi yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari Mkuu
wa Kitengo Cha Utafiti na ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi
ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni
sehemu ya utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za
viwandani na majumbani sura 182.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 matukio ya kemikali yalisababisha vifo 14.
“Jumla ya
matukio 11 ya ajali za Kemikali yalitolewa taarifa katika kipindi cha
mwaka jana pekee na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua
moto magari na tani 250 za kemikali”.alisisitiza Mallya.
Akifafanua
kuhusu matukio hayo Mallya amesema kuwa ajali hizo zilisababishwa na
kukosekana kwa uelewa juu ya athari zinazoweza kusababishwa na kemikali
hizo miongoni mwa wasafirishaji na watumiaji.
Kama
sehemu ya utekelezaji wa sheria hii,Serikali inatarajia kuendelea
kufanya mafunzo ya wadau kuhusiana na kemikali zenye kusababisha
mlipuko.
Mafunzo
hayo yatatolewa kwa wakuu wa polisi wa Usalama barabarani nchi nzima
yanalenga kuongeza uelewa kwa wadau wanaohusika katik a kutumia na
kusafirisha kemikali ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.
Katika
kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yasiliyo salama,ajali na
matukio ya kemikali,Serikali iliamua kutunga sheria ya usimamizi na
udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura 182 (The Industrial
and Consumer Chemicals Management and Control) Act Capt 182).
Lengo kuu
la sheria hii ni kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyo
salama bila kuleta athari kwa watu na mazingira.
0 comments: