MKamishna
Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na
waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei
2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa
Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.
Abdul Mapembe.
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni
1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la
kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo.
Makusanyo
ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla
ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi
trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na
Zanzibar.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya
mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea
na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo
iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na
kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka
katika ukusanyaji wa mapato.
“TRA
imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi
mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa
fedha, ambapo kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo hususani
katika pwani ya bahari ya Hindi na mipaka yote, kupambana na
wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za
kodi za keielektroniki , kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu
pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi
mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema Kamishna
Mkuu.
Bw.
Kidata ameendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo
kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza
bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.
Katika
kutekeleza agizo la Mh. Rais na kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa
ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD Mamlaka imeanza
utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za EFD kwa
wafanyabiashara wadogo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
TRA
imeanza ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wapatao 5,703
wenye mauzo ghafi kati ya Shilingi milioni 14 na milioni ishirini (20)
kwa mwaka, wafanyabiashara hao wanatakiwa wafike katika ofisi za Mamlaka
ya Mapato za Mikoa wanayolipia kodi ya Ilala, Kinondoni na Temeke ili
waweze kuhakiki usajili wao wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
na kupewa kibali cha kupewa Mashine ya EFD zoezi lililoanza Juni Mosi
alisisitiza Kamishana Mkuu.
Aidha,
Bw. Kidata alifafanua kuwa zoezi hili litaendelea katika Mikoa yote
Tanzania kwa awamu kwa utaratibu utakaotangazwa mara kwa mara na hivyo
kutoa wito kwa wafanyabiashara wenye mauzo tajwa wote nchini kutoa
ushirikiano pindi inapofika zamu yao katika Mikoa yao.
Zoezi
hili litasaidia kuongezaka kwa Mapato ya nchi endapo wafanyabiashara na
wananchi watakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha wanatumia mashine
hizo na kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu wafanyabiashara wote watakao
kiuka kutumia mashine hizo za EFD.
Kwa
upande wa wananchi, kamshna mkuu amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo
bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia
sambamba na risiti walizopewa .
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
0 comments: