Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akifafanua jambo wakati
wa majumuisho ya mkutano wa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme
vijijini inayofadhiliwa na Wakala
wa Nishati Vijijini (REA),(hawapo pichani). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Juliana Pallangyo.
Mkurugenzi
wa ufundi wa Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Mhandisi Bengiel Msofe akifafanua jambo wakati wa majumuisho ya mkutano wa wakandarasi
wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini
inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini,(REA). Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo na katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini anayeshughulikia nishati Dk. Juliana Pallangyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Juliana
Pallangyo( katikati) akieleza jambo wakati wa majumuisho ya mkutano wa
wakandarasi wanaotekeleza miradi ya
umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini,(REA). Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo na kulia ni Mkurugenzi wa ufundi
wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mhandisi Bengiel Msofe.
Sehemu
ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini,(REA) na wanahabari, wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa
inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( hayupo
pichani).
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo amesema kuwa kwa Tanzania
kutopatiwa fedha na Marekani kupitia Mfuko wa Maendeleo
ya Changamoto za Milenia (MCC) ambazo ni Dola za Marekani milioni 472 kwa ajili ya miradi ya barabara,
maji na umeme hazitaathiri miradi
ya usambazaji umeme vijijini
inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Aliyasema
hayo jijini Dar es salaam wakati akifanya majumuisho ya vikao vyake na wakandarasi wanaosambaza
umeme vijijini ambavyo vilianza tarehe 29 Machi, 2016 na kuhudhuriwa na watendaji wa
Wizara, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na REA.
Profesa
Muhongo alisema kuwa fedha hizo zilikuwa haziendi moja kwa moja katika mfuko wa
REA wala serikali kuu kama inavyodaiwa na watu wengi.
“Zile
fedha za MCC tulikuwa tunakaa na MCC, tunasema bwana katusaidie kusambaza umeme
mfano Shinyanga, kwa hiyo anachukua zile fedha zake anaenda na wakandarasi wake
moja kwa moja Shinyanga, huku miradi ya REA ikiendela kama ilivyopangwa, ” alisema
Profesa Muhongo.
Alisema
kuwa miradi ya MCC ilikuwa ikisaidia juhudi za serikali katika kusambaza
umeme vijijini na mijini lakini fedha hizo
zilikuwa hazipelekwi REA.
Alisisitiza
kuwa kabla ya MCC kuanza kutoa fedha za kuendeleza miradi ya umeme,
serikali tayari ilikwishaanza
kusambaza nishati hiyo kwa wananchi na
kwamba kuna wadau mbalimbali
wanaochangia miradi hiyo na hata kama
wasipochangia, jukumu la serikali
la kuwasambazia wananchi
wake umeme linabaki kuwa pale pale.
“Isichukuliwe
kwamba fulani asipochangia, sasa taifa zima miradi yake imekufa, hivyo dhana ya
kusema kwamba fedha hizo zilikuwa zinapelekwa REA ni upotoshwaji wa hali ya
juu, kwamba REA itaathirika kwa kukosa hizo
fedha si kweli,” alisema Profesa Muhongo.
Akielezea
utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya pili, Profesa Muhongo alisema awali jumla
ya shilingi bilioni 881 zilitengwa lakini zikaongezeka shilingi bilioni 60
ambapo hadi kukamilika kwa awamu hiyo ya
pili jumla ya vijiji 2500 vinatarajiwa
kupata umeme, huku wateja wa awali 250, 000
kuunganishwa na huduma hiyo hadi
kufikia mwezi Juni, mwaka huu ambao ni ukomo wa utekelezaji wa awamu hiyo.
Kuhusu
tathmini
ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini, Profesa Muhongo alisema
kuwa wakandarasi wengi wametekeleza miradi hiyo kwa asilimia kati ya 75
na 85, huku wengine wakivuka wastani wa REA ambao ni asilimia 87.
Katika
hatua nyingine, Profesa Muhongo alitoa miezi miwili kwa wakandarasi ambao
hawajakamilisha miradi na kusisitiza
miradi yote kukamilishwa mwezi Mei au
Juni 15, mwaka huu kabla ya
kuanza kwa awamu ya tatu inayotarajiwa kuanza ifikapo Julai mosi mwaka huu.
Aliongeza
kuwa
katika utekelezaji wa miradi ya
umeme vijijini, serikali imebaini
kuwa wapo wakandarasi wanaotumia vifaa hafifu kama transfoma na nguzo
na kusisitiza ukaguzi kufanyika na kampuni itakayobainika
kutumia vifaa hafifu itafutwa mara moja kabla
ya awamu ya tatu.
Ili
kutekeleza
miradi hiyo kwa ufanisi, Profesa Muhongo aliitaka TANESCO kwa
kushirikiana na Wizara kuhamasisha wananchi hasa waishio vijijini
kujiunga na huduma ya umeme,
na TANESCO kusogeza huduma
karibu na wananchi ili kuepusha wananchi
kusafiri umbali mrefu kufuata
huduma ya kuunganishiwa umeme au changamoto nyingine zinazotokana na
nishati
hiyo.
Akizungumzia
kuhusu malipo ya wakandarasi hao, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali
imeendelea kulipa wakandarasi wote kwa wakati kulingana kazi zinazofanyika.
Wakati
huo
huo Profesa Muhongo alisema kuwa mitambo ya kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I kwa sasa inazalisha Megawati 150 na
kuongeza
kuwa malipo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi II inayojengwa
na
kampuni ya Sumitomo kutoka nchini Japan yameshakamilika
0 comments: