Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua ujenzi wa jengo la
upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala ambalo litakuwa maalumu kwa
ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine
wadharura.
Jengo
hilo ambalo ujenzi wake utaanza rasmi kesho, litakuwa na vyumba maalumu
kwa ajili ya upasuaji, uangalizi maalumu kwa ajili ya wagonjwa
wadharura (ICU) na uangalizi baada ya upasuaji na vingine kwa ajili ya
utawala na huduma nyinginezo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam leo mchana DC Makonda alisema
kuwa jengo hilo litakuwa mahususi kwa ajili ya kupunguza idadi ya
wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji kwenda Hospitali yaTaifa ya
Rufaa yaMuhimbili.
“Kupitia
jengo hili wajawazito wote na wagonjwa wengine ambao wanahitaji
upasuaji watapatiwa huduma hiyo hapa hapa Mwananyamala.
Alisema
jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa 350-360 hivyo
kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumepunguza msongamano Muhimbili.
Pia
utakuwa tumefanikiwa kuokoa maisha ya wajawazito ambayo yameku wa
yakipotea kutokana na kuchelewa kupata tiba,” alisemaMakonda.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa yaKinondoni, Dk. Azizi Msuya
alisema jengo hilo litasaidia kuokoa maisha ya wajawazito na wagonjwa
wengine ambao wamekuwa wakifariki kutokana na kucheleweshewa kupata
huduma hizo.
“Katika
wajawazito 100,000 wanaojifungua, 447 wanapoteza maisha. Sasa kupitia
uwepo wa huduma ya upasuaji katika hospitali hii ya Mwananyamala
tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha ya wajawazito hao
wanaofariki” alisemaDkAzizi.
Mwakilishi
wa Kampuni ya GSM Foundation ambao ndiyo wafadhili wa ujenzi wa jengo
hilo, Deogratias Ndejembi alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kufadhili
ujenzi huo ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipoteza
maisha kutokana na kukosa huduma ya upasuaji na pia kutokana nakuguswa
na juhudi za DC Makonda.
“Kama
GSM tumeamua kugharamia ujenzi wa jengo hili la upasuaji ili kuokoa
maisha ya wanawake, watoto na jamii nyingine ambayo imekuwa ikipoteza
maisha kwa kukosa upasuaji. Pia juhudi na uchapaji kazi wa DC Makonda. Amekuwa akifanya kazi kwa juhudi kubwa, hivyo tukaona ni vyema tuka muunga mkono” alisema Deogratias Ndejembi.
DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM mbele ya msingi litakapo jengwa jengo hilo.
Ukataji utepe ukiendelea.
DC Makonda akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa ujenzi huo.
DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM Foundation. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya.
DC Makonda akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi huo.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya akizungumza na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa za ujenzi huo.
0 comments: