NiceMediaWorks
Home
Posts
Email
MATUKIO
HABARI
MAGAZETI
MAKALA
BURUDANI
AFYA
PRODUCTION
INJILI
Style Icons
MAWASILIANO
Top 10 List
Monday, November 2, 2015
CHADEMA YAKANUSHA KUHUSU HABARI INAYOENEA MTANDAONI KUWA WAMEISHTAKI NEC ICJ
at 3:04:00 AM | 
No comments
SalaamZiko habari zimezushwa, kuenezwa na sasa zinakuzwa kuwa mgombea urais wa CHADEMA na chama kwa ujumla kimefungua shauri Mahakama za Kimataifa, kuhusu ubakwaji wa demokrasia na hujuma dhidi ya Watanzania uliofanyika kwenye Uchaguzi (uchafuzi?) Mkuu uliofanyika Oktoba 25.Itoshe tu kusema kuwa hadi kwa hatua ya sasa habari hizo si za kweli. Ni uzushi.Watawala, wanaotuhumiwa kupoka haki ya Watanzania ya kuchagua viongozi wanaowataka, wanajua dhambi waliyowafanyia wananchi ni sawa na ile hadithi ya Mzee Mvuvi kwenye Vitabu vya Alfu Lela Ulela, aliyefungulia jini kutoka kwenye chupa. Dhambi inawawinda. Mzimu wa walichokifanya unawaandama. Maana safari hii ukatili (kuvuruga uchaguzi) ulikuwa wazi wazi mno.Wanajaribu kuchokonoa kujua ukimya wa Ndugu Edward Lowassa, kama mgombea chaguo la watu, CHADEMA, UKAWA na wapenda mabadiliko unaweza kuwa na kishindo gani! ICJ, ICC au wapi hasa!Hivyo wanatunga tunga mambo na kusambaza wakitaka kupima hisia, fikra za wanamabadiliko waliotapakaa nchi nzima wakilia kilio cha kudhulumiwa haki katika uchaguzi, zinawaza nini! Maana hata wao wanashuhudia namna nchi ilivyokumbwa na msiba tangu walipotangaza matokeo yasiyooana na uhalisia wa hisia za wapiga kura na matakwa ya waliyo wengi katika demokrasia.Tumelazimika kufafanua kuhusu uvumi huo kwa sababu umezidi kuenezwa kiasi cha vyombo vya habari kuanza kuulizia ukweli wake.Baadhi ya watu waliotajwa kwa majina katika uvumi huo wako hapa nchini, wakiendelea na majukumu, hususan vikao vya Kamati Kuu ya dharura, ambayo imekuwa ikikutana jijini Dar es Salaam.Chama kilipoandika barua kwenda Jumuiya ya Kimataifa, kuhusu hatari iliyokuwa inawekwa na watawala katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupitia kauli za vitisho, matendo yao ya kujiandaa kuharibu uchaguzi, BVR, mfumo wa ujumlishaji matokeo n.k, tuliutaarifu umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari. Kwa sababu si siri.Ukifanywa uamuzi mwingine wowote ule kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania kupigania haki yao iliyoporwa katika uchaguzi mkuu, umma wa Watanzania ambao ndiyo wenye mamlaka katika nchi, utashirikishwa
.Makene
Share
MATUKIO
Posted by Unknown
About the Author
Write admin description here..
«Newer Post
Older Post»
0 comments:
About Me
Unknown
View my complete profile
NiceMedia. Powered by
Blogger
.
BOFYA HAPA LIVE NICEMEDIA RADIO
Radio ya Injili inayoburudisha na Kuelimisha
Popular
Recent
Comments
Tags
Popular Posts
NICE STUDIO YA JIJINI ARUSHA YAPANIA KUWAINUA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI.Tazama hapa.....
SERIKALI YA KOREA YAGHARAMIA UJENZI WA HOSPITAL YA CHANIKA UTAKAO GHARIMU BILIONI 8.8 ZA KITANZANIA
TANZNIA YAPIGA HATUA KIUCHUMI ASEMA WAZIRI MKUU
Mkutano wa Ulaya na Afrika waanza Brussels
MTU YOYOTE YULE ANAWEZA KUWA BINGWA KATIKA JAMBO LOLOTE ALITAKALO
Labels
Afya
BURUDANI
Favourite
Gear
HABARI
HABARI ZA INJILI
HIVI PUNDE
MAGAZETI
MAKALA
MATUKIO
nice studio
SIASA
slider
TANGAZO
Nice Media work Tz
Latest tweets
Latest Videos From NiceMedia Prod.
Search
BLOG RAFIKI
Udaku Special
MillardAyo
Jiachie
Text Widget
© 2013
NiceMediaWorks
.
Woo Themes
converted by
Bloggertheme9
Blogger templates
. Proudly Powered by
Blogger
.
0 comments: