Mwili wa marehemu Edga Milinga ukiwa umewekwa kwenye gari la polisi. |
Mandhari ya kituo cha polisi kilichovamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo. |
Habari zilizotawala katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ni kwamba mnamo usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane za usiku Majambazi wasiojulikana idadi walivamia kituo cha polisi Ikwiriri na kuwauwa askari polisi wawili waliokuwa zamu ambao ni askari mwenye namba E.8732 CPL Edga Milinga na WP 5558 PC Judith Timoth.
Majambazi hayo yalifanikiwa yalifanikiwa kupora silaha saba 7 ambapo ni SMG 2, SAR 3, Ant Rayot 1, ambazo zote ni mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na silaha 1 aina ya Short Gun Protector mali ya kampuni ya sigara Tanzania.
Majambazi hayo yalifanya uharibifu mkubwa baada ya kulipiga risasi gari la Polisi lenye namba PT 1965 na kulichakaza kabisa...
0 comments: